Mabilioni yapotea kwa kutotumia vizuri mikataba ya biashara huru, FTAs

29 Januari 2018

Ripoti mpya iliyotolewa leo imeonyesha kuwa bado kuna shida kubwa katika matumizi sahihi ya mikataba ya biashara huria ambayo Muungano wa Ulaya imetia saini na nchi zingine.

Matumizi yasiyotosheleza ya mikataba hiyo husababisha kupotea kwa dola takribani bilioni 89, imesema ripoti hiyo iliandaliwa kwa pamoja na kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD na bodi ya taifa ya biashara ya Sweden.

Miongoni mwa vikwazo vilivyotajwa ni kanuni ya kuthibitisha eneo halisi ambako bidhaa imetoka, kigezo ambacho ndio kinahalalisha bidhaa kunufaika na mikataba ya biashara huria.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi katika utangulizi wa ripoti hiyo amesema takwimu hizo za matumizi yasiyoridhisha ya mikataba hiyo zinatoa changamoto kuhusu fikra potofu uchaguzi wa bidhaa katika mikataba hiyo.

Ripoti inasema dhana ya viwango vya matumizi ya mikataba hiyo inaweza kutumiwa na watunga sera wa nchi zinazoendelea hasa katika kufuatilia biashara kati ya nchi za kusini, ikitaja zaidi nchi za Afrika wakati huu ambapo zinajadili mikataba ya biashara huria baina ya mabara.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud