Usugu wa viuavijasumu ni tishio duniani kote:WHO

29 Januari 2018

Takwimu zilizotolewa leo na shirika la afya duniani WHO kuhusu usugu wa viuavijasumu au antibiotics zinaonyesha kwamba kiwango cha usugu wa dawa hizo dhidi ya maradhi kadhaa yanayosababishwa na bakteria au vimelea kiko juu katika nchi zote, za kipato cha juu , cha wastani na za kipato cha chini. Taarifa kamili na Assumpta Massoi

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Kwa mujibu wa mfumo mpya wa WHO wa ufuatiliaji wa kupambana na vijiumbe maradhi au antimicrobial ujulikanao kama (GLASS), takwimu hizo zimekusanywa kwa watu 500,000 walioathirika na vimelea na kutumia dawa kutoka nchi 22.

Ripoti inasema kuna takribani vimelea saba ambavyo ni sugu dhidi ya dawa za viuavijasumu vikiwemo Staphylococcus(STAFILOKOKAS) , E.coli (IKOLAI) na salmonella (SALIMONELA) ingawa ripoti hiyo haijajumuisha takwimu za vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

WHO inasema takwimu hizo zinathibitisha tatizo kubwa kote duniani. Hadi sasa kuna nchi 52 zilizoathirika na tatizo hili , 25 za kipato cha juu, 20 za kipato cha wastani na 7 za kipato cha chini ambazo zimeorodheshwa katika mfumo wa GLASS wa WHO. Dr Regina Mbindyo ni afisa wa WHO nchini Kenya anasema kwa upande wa Afrika na hasa Kenya

(SAUTI YA DR REGINA MBINDYO)

WHO imeongeza kuwa ripoti hii ni hatua ya kwanza muhimu kuelekea kuboresha uelewa kuhusu kiwango cha usugu wa viuajisasumu na kisha kuchukua hatua madhubuti dhidi ya tishio hilo kubwa la kimataifa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud