Elimu ndio muarobaini dhidi ya chuki za kibaguzi

Elimu ndio muarobaini dhidi ya chuki za kibaguzi

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi, Umoja wa Mataifa umesema silaha pekee dhidi ya vitendo kama hivyo ni elimu na uelewa kuhusu maadili ya kibinadamu.

Katibu Muu wa Umoj awa Mataifa António  Guterres amesema hayo katika ujumbe wake akieleza kuwa mambo hayo ni muhimu hivi sasa kwa kuwa hata baada ya vita kuu ya pili ya dunia, bado kuna mwendelezo wa chuki siyo tu dhidi ya wayahudi bali pia chuki kwa misingi mingine kama rangi na dini.

Ametolea mfano vikundi vya kibaguzi kwa misingi ya Unazi mamboleo na vile vinavyotaka heshima na utambuzi wa juu kwa watu weupe akisema vikundi hivi ni wapeperushaji wa bendera za chuki iliyopita kipimo.

Bwana Guterres amesema na jambo baya zaidi, fikra hizo zinatoka pembezoni na kujumuishwa kwenye masuala ya jamii na siasa.

Hivyo basi katika siku hii ya kukumbuka wayahudi milioni 6 waliouawa wakati wa mauaji ya halaiki, Bwana Guterres ametoa wito kwa kila mkazi wa dunia kuwajibika bayana na kupinga ubaguzi wa rangi, ghasia na ukiukwaji wa haki kwa misingi yoyote ile.

Photo Credit
Kumbukizi ya mauaij ya halaiki ya wayahudi. (Picha:UN/Maktaba)