Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zahma ya Libya yahitaji dfola milioni 313 mwaka huu

Zahma ya Libya yahitaji dfola milioni 313 mwaka huu

Pakua

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, amezindua mkakati wa kushughulikia zahma ya kibinadamu mwaka  huu wa 2018 nchini  Libya.

Mpango huo uliozinduliwa na Bi Maria Ribeiro unalenga kuchangisha dola millioni 313 za kutumiwa kwa ajili ya msaada kwa 2018 ili kuokoa maisha ya watu   940,000.

Mpango  mkakati huo (HRP) umezinduliwa kwa niaba ya jumuiya ya wahisani wa misaada ya kibinadamu kwa ushirikiano na wakuu wa mamlaka ya Libya.

Ombi hili ni la tatu kutolewa na litasaidia kutekeleza  miradi 71, inayoendeshwa na asas iza kiraia 22 mkiwemo  mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza  wakati wa uzinduzi, Bi. Riberio, amesema wananchi wa Libya hupitia matatizo makubwa, kupata mahitaji muhimu na kuongeza kuwa ni sharti wawe chonjo dhidi ya athari za kutofanya jambo lolote kuhusu hali hiyo.

Miradi hii ina nia ya kutoa ulinzi kwa raia wa kawaida, kulingana na  sheria za kimataifa, ili kuhakikisha kuwa watu wanapata huduma bora mfano wakimbizi wa ndani, watu wanaorejea kutoka ukimbizi au uhamishoni pamoja na raia walioko Libya ambao hawakupoteza makazi yao kama vile wahamiaji, wakimbizi na watafuta hifadhi.

Fedha hizo pia zitasaidia familia kupata uwezo wa kukidhi maisha yao dhidi ya shinikizo zinazoendelea za kuporomoka kwa uchumi, mparaganyiko wa familia pamoja na hali ya kukosekana  kwa amani.

Takriban watu millioni 1.1 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini humo.

Photo Credit
Mama na mtoto wake nchini Libya. Picha: UNFPA