Vifo vya watoto wachanga Nyarugusu vyatia hofu

25 Januari 2018

Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linahaha kusaidia hospitali ya Nyarugusu mkoani Kigoma ili iweze kuboresha huduma zake ili hatimaye kupunguza vifo vya watoto wachanga. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Nats..

Ndani ya moja ya wodi za hospitali ya Nyarugusu nchini Tanzania, mtoto mchanga aliyezaliwa njiti, ikiwa ni wiki nane kabla ya muda wake wa kuzaliwa, akiwa kwenye mashine ya kumwezesha kupumua ili aweze kuishi.

image
Mtoto aliezaliwa wiki nane kabla ya wakati wake katika hospitali ya Nyarugusu nchini Tanzania. Picha: UNHCR/Video capture

Yeye amebahatika kwani katika hospitali hii inayohudumia wakimbizi na wenyeji kiwango cha vifo vya watoto wachanga kinatia wasiwasi kwani kuna uhaba wa wafanyakazi, dawa na vifaa.Susana Kahoto ni mama ambaye mtoto wake mchanga alifariki dunia kwenye hospitali hii..

(Sauti ya Susana Kahoto)

Dkt. Florence Mshana ni Mkurugenzi wa hospitali hii ambayo ni tegemeo kubwa kwa wakimbizi 150,000 wa kambi ya nyarugusu wengi wao wakiwa ni watoto.

(Sauti ya Dkt. Florence Mshana)

“Kwa wastani kuna vizazi kati ya 550 hadi 600 kwa mwezi. Wakati mwingine watoto waliozaliwa wanahitaji usaidizi wa kupumua tu wanapozaliwa au mashine kwa wale waliozaliwa njiti. Wanahitaji kuwekwa kwenye kitengo cha watoto njiti, tunahitaji vifaa vya kuwapatia joto, pia eneo la kuwatunza watoto njiti.”

Kufuatia uhaba huo wa vifaa na huduma kwa wajawazito, UNHCR imeamua kufadhili ujenzi wa wodi mpya ya wazazi, ingawa shirika hilo limesema fedha zaidi zinahitajika ili kuokoa maisha ya watoto.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud