Kazi ni kazi bora mkono uende kinywani
Pakua
Vijana hutumia mbinu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya maisha yao ya kila siku na fani ya ulimbwende au uanamitindo imekuwa ni moja ya fani zinazowavutia vijana , kwanza ikiwajengea umaarufu mkubwa lakini pia kuwasaidia kuwa na ajira ya kikidhi mahitaji yao. Hakimu Nkengurutse kijana wa miaka 21 kutoka vijijini nchini Burundi amevuka mito na bahari na kutua nchini Afrika ya Kusini ambako anakofanya kazi ya uanamitindo.
Na baada ya kufanikiwa kwenye kazi hiyo, Hakim sasa anatumia muda wa mapumziko katika nchi yake ya asili Burundi ili kuwachagiza vijana wenzie kuchangamkia faini hiyo ambayo imegeuza Maisha yake. Kufahamu zaidi safari ya mafanikio yake ungana na mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA katika Makala hii.