Skip to main content

Guterres akutana na waasi wa zamani wa FARC Colombia

Guterres akutana na waasi wa zamani wa FARC Colombia

Pakua

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametembelea iliyokuwa  ngome ya waasi wa FARC  huko mji wa Mesetas, Meta colombia na kujionea mchakato wa maendeleo ya waliokuwa wana mgambo wa kundi hilo.

Akiwa ziarani nchini Colombia, bwana Guterrres amekutana na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa dini, asasi za kiaraia na pia viongozi wa kundi la FARC, ambalo zamani walikuwa ni wanamgambo nchini humo.

Akiwa katika ngome FARC Mesetas Meta, bwana Guterres amepongeza juhudi zinazofanywa na  waasi hao wa zamani wa FARC nchini huo za kuendeleza mchakato wa amani akisema….

(Sauti ya Antonio Guterres)

"Jamii inaamini kwamba inawezekana kwa mkoa huu kufikia sio amani tu, bali pia maendeleo  na mazingira mazuri ya kuishi kwa wakazi wake wote, na kwamba Serikali ya Colombia itachukua  jukumu muhimu katika kuhakikisha usalama, utawala bora na pia mfumo wa huduma bora za afya na miundombinu kwa wananchi wake katika kusaidia wakulima wa ndani kupata  maendeleo."

Bwana Guterres amesema, ahadi ya Umoja wa Mataifa iko paleplae katika  kusaidia kwa hali na mahali mchakato wa amani, maendeleo na utawala bora  chini colombia.

Photo Credit
Katibu mkuu Guterres akisalimiana na wanakijiji wa Mesetas, Meta baada ya kuwasili.