Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nishati ya jua yaleta nuru kwa wakimbizi Angola

Nishati ya jua yaleta nuru kwa wakimbizi Angola

Pakua

Esther, mwenye umri wa miaka 25 aliishi kwa amani na furaha na familia yake huko Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, lakini ghafla akajikutaka akilazimika kuacha kila  kitu chake na kukimbilia yeye na familia yake nchini Angola. Kulikoni? Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Kwa bahati nzuri alifika mefanikiwa kufika katika kambi ya wakimbizi ya Louva nchini Angola ambapo hapa anakutana na wakimbizi wenzake zaidi ya 35,000 kati yao asilimia 75 ni wakinamama na watoto. Kambi hii ipo porini na hivyo jua likizana hakuna mwanga , kiza totoro.

Hali hii inaleta hofu nyingine hasa kwa wanawake wanaotaka kujifungua hata mahitaji ya kujihifadhi ya kawaida kwa mwanamke akiwa katika hedhi, tena ni changamoto kubwa kutembea usiku kwakuwa wengi wahofia kubakwa.

Shirika la Idadi ya watu ulimwenguni UNFPA kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la Japan wameliona hili na kuamua kutoa Taa 50 zinazotumia nishati ya jua kwa jili ya kusaidia wahitaji kama Ester.

Akikabidhi msaada huo mwakilishi wa UNFPA nchini Angola Florbela Fernandes amesema mwanga ni muhimu katika kuendelea kuhakikisha kuna usalama lakini pia ni haki ya wanawake na wasichana suala lililoungwa mkono na Yuzo Kitamoto kutoka JAPAN.

image
Wataalamu kutoka Japan ambao wanasimamia mradi huo wa nishati ya jua wakikagua mtambo katika moja ya hema kambini Louvua nchini Angola. © UNFPA/Tiril Skarstein)
 
Photo Credit
Ester na wanae walikimbia ghasia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC sasa hapa kwenye kambi ya Lóvua nchini Angola, japo ni ugenini angalau sasa kuna matumaini. (Picha: © UNFPA/Tiril Skarstein)