Ndege zisizo na rubani zasafirisha damu Rwanda

Ndege zisizo na rubani zasafirisha damu Rwanda

Pakua

Katika ajenda ya maendeleo endelevu SDGs ya mwaka 2030, lengo namba 3 la afya bora kwa kila mtu, limekuwa changamoto kubwa sana hasa kwa nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.

Umoja wa Mataifa na washirika wake katika masuala ya afya wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma ya elimu na pia  misaada kwa serikali mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na kuziwezesha katika sekta ya afya.
Nchini Rwanda hali ni tofauti , kwani serikali ya nchi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta ya afya hususan katika kutoa huduma bora na ya haraka ya damu katika hospitali mbalimbali.
Mwandishi wetu Patrick Newman alipata fursa ya kuangazia jinsi teknolojia mpya  ya ndege isiyokuwa na rubani kwa kingereza drone,  inavyotumiwa kusambaza damu kwa haraka katika vituo vya afya nchini humo.
Photo Credit
Kijana mfanyakazi wa kampuni ya Zipline inayotengeza ndege sizizokua na rubani aina ya drone kigali Rwanda.