Teknolojia kubaini uimara wa majengo Mexico

28 Disemba 2017

Tarehe 20 mwezi septemba mwaka huu 2017 mji wa Mexico nchini Mexico ulikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 katika kipimo vya richa na kusababisha vifo vya Zaidi ya watu 200 na kuharibu mamia ya majengo.

Miezi mitano baada ya tetemeko hilo mji wa mexico ukiwa umebaki na majengo mabovu yaliyoathirika, viongozi wanashauriwa kutobomoa kwa kuwa imepatikana teknolojia mpya ya kubaini uimara au udhaifu wake.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Mexico kutumia teknolojia hiyo mpya ambapo mhandihi Abel Domato kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA anasema..

image
Kifaa cha kupima kiwango cha uharibifu wa majengo.(Picha:Unifeed Video capture)

(Sauti ya Abel Domato)“Mbinu zisizo haribifu za uchunguzi zinatuwezesha kupata mawazo ya juu zaidi ya jingo na mchanganyiko wake.

Naye Lydia Paredes mkurugenzi kutoka taasisi ya utafiti wa nyuklia nchini Mexico amesema wanataka kufanya utafiti wa haraka na uhakika ili kubaini majengo hatarishi kwa jamii.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud