Uchaguzi mkuu Liberia, UN yatuma mwakilishi wake

Uchaguzi mkuu Liberia, UN yatuma mwakilishi wake

Pakua

Duru ya pili ya uchaguzi nchini Liberia imefanyika hapo jana.

Kufuatia kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi wa Rais nchini Liberia, Umoja wa mataifa ambao umekuwa ukishirikiana na nchi hiyo katika kuhakikisha amani na utulivu imemmtuma msuluhishi wake kwenda nchini humo.

Msuluhishi huyo ni Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo ambaye amekuwa akifanya jukumu la upatanishi nchini humo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa Obasanjo atakuwa nchini Liberia kuanzia tarehe 28 hadi 30 Disemba mwaka huu 2017 ili kuangalia namna uchaguzi huo unavyomalizika na mshindi anakabidhiwa madaraka katika muda uliopangwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Halikadhalika Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa ameipongeza  serikali ya Liberia ,wanasiasa na  wananchi kwa kuendeleza amani katika kipindi chote cha kampeni mpaka kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi baada ya ile ya kwanza kushindwa kumpata rais kwa mujibu wa katiba yao na kueleza kuwa na matumaini wataendeleza hali hiyo hata baada ya mshindi kupatikana na kutangazwa muda wowote kuanzia sasa.

Photo Credit
Nchini Liberia mwananchi akipiga kura huku wasimamizi wakifuatilia kwa karibu. (Picha:UNDP/Liberia)