Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru zaidi yaangazia wakimbizi walioko korokoroni Libya

Nuru zaidi yaangazia wakimbizi walioko korokoroni Libya

Pakua

Harakati za kuhamisha kutoka Libya wakimbizi walio hatarini zaidi zinaendelea chini  ya usimamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Katika hatua ya hivi karibuni zaidi wakimbizi 162 walisafirishwa kwenye Roma, Italia kwa kutumia ndege mbili.

Miongoni mwao ni wanawake, watu wenye ulemavu na watoto waliokuwa wanashikiliwa mateka wakiwa na hali mbaya zaidi.

UNHCR imesema wanawake watano kati yao wakati wanashikiliwa mateka walijifungua watoto bila usaidizi wa kutosha wa matibabu.

Uraia wao ni pamoja na Somlia, Eritrea, Ethiopia na Yemen ambapo UNHCR imesema wakimbizi wanasindikizwa hadi Tripoli na hatimaye Roma, italia ambapo wanapokelewa katika kituo cha kijeshi kabla ya kukabidhiwa kwa mamlaka husika za uhamiaji za Italia.

UNHCR imesema mara baada ya kuwasili Roma, wahamiaji hao wamefanyiwa uchunguzi wa afya zao na kupatiwa nguo, mlo wa moto na malazi na ndipo taratibu za uhamiaji zikafuata.

Photo Credit
Wakimbizi wahamishwa kutoka Libya kwenda Italia. (Picha:UNifeed Video Capture)