Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili na mauaji vyaendelea Sudani Kusini- Ripoti

Ukatili na mauaji vyaendelea Sudani Kusini- Ripoti

Pakua

Ripoti ya watalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa wiki hii imesema baada ya miaka minne ya  machafuko nchini Sudan Kusini imebanika kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na pande kinzani uliosababisha maisha ya watu wengi wasio na hatia kupotea.

Wataalamu hao  walifanya  uchunguzi kwa ushirikiano na IGAD, nchini Sudan Kusini, Mashariki mwa Ethiopia na kaskazini mwa Uganda kuanzia tarehe 11 had 22 Disemba  na kuwasilisha ripoti hiyo huko Addis Ababa.

Ripoti imebaini  kuwepo na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo vitendo vya utekwaji nyara kwa watoto, ubakaji kwa wanawake na wasichana, mauaji, uporaji wa mali za wananchi, uchomwaji wa makazi ya watu na pia ukimibizi wa ndani  kwa mamilioni ya raia.

Profesa Andrew  Claphan wa ofisi ya haki za binadamu  amesema walishtushwa na ushahidi  kutoka kwa  waathirika wakati wakitembelea Sudan Kusini katika jitihada za kukusanya taarifa kwa waathirika wa ukatili hususan wanawake walipokuwa wanaeleza kuhusu vitendo vya ubakaji walivyofanyiwa.

Ofisi ya haki za binadamu imetoa wito kwa pande  zote kinzani kusitisha mapigano  mara moja na kukaa kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya kutafuta suluhisho la mgogoro huu ili kuokoa maisha ya mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia na pia kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie walengwa..

Photo Credit
Uthibitisho wa ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini (Picha:UNMISS/Nektarios Markogiannis)