Buriani!

14 Disemba 2017

Leo imekuwa ni siku ya huzuni na majonzi makubwa nchini Tanzania ambako serikali, jeshi na wananchi na Umoja wa mataifa wamejumuika jijini Dar es salaam kuwaenzi na kuwapa mkono wa kwaheri mashujaa 14 walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini humo waliouawa katika shambulio la wiki iliyopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Leah Mushi na tarifa kamili

(TAARIFA YA LEAH MUSHI)

Natts…..

Mkuu wa Opresheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa bwana Jean-Pierre Lacroix atia saini kitabu cha wageni katika sherehe za kuaga walinda amani Tanzania. Picha: UN

Tukio hilo lililoighubika Tanzania na simanzi kubwa limeambatana na sala, hotuba na utoaji heshima za mwisho kwa wanajeshi hao kabla ya kusafirishwa kwa mazishi, limeongozwa na waziri mkuu wa Tanzania Bwana Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo familia za marehemu, viongozi wa serikali, mashirika, wanajamii, na Umoja wa Mataifa ambao umewakilishwa na mkuu wa Opresheni za ulinzi wa amani za Umoja huo bwana Jean-Pierre Lacroix.

(SAUTI YA JEAN-PIERRE LACROIX )

"Nimekuja hapa kutoa rambirambi zetu kwa serikali , watu wa Tanzania na familia za walinda amani  hao  14 kutoka Tanzania waliouawa na pia kutoa shukrani za dhati za Umoja wa Mataifa kwa Tanzania kwa uwajibikaji wao mkubwa katika masula ya amani na hususani ulinzi wa amani”

Jamii na raia waaga walinda amani nchini Tanzania. Picha: UM

Akizungumzia pigo hilo sio tu kwa Tanzania bali kwa jumuiya ya kimataifa na hususani operesheni za ulinzi wa amani waziri Mkuu bwana Majaliwa amesisitiza haja ya uchunguzi wa kina

(SAUTI YA KASSIM MAJALIWA )

Akiunga mkono hoja hiyo kwa niaba ya Umoja wa Mataifa bwana Lacroix amesema

Viongozi mbalimbali wa Jumuiya wa Kimataifa pamoja na wanajeshi waomboleza na wananchi wa Tanzania. Picha: UM

(SAUTI YA JEAN-PIERRE LACROIX -2)

"Kutakuwa na uchunguzi wa nini kilichotokea , nini lkilichosababisha tukio hilo, bado ni mapema sana kufikia hitimisho lolote tunashirikiana na serikali ya Tanzania na nchi nyingine wachangiaji wa vikosi, ili kubaini nini hasa kimlichotokea na hatua gani tunaweza kuchukua pamoja ili kuwalinda vyema askari wetu na raia tunaowahudumia"

Kati ya wanajeshi hao 14 waliouawa baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na kundi la waasi la ADF huko Kivu ya Kaskazini 12 wanatoka kisiwani Zanzina na wawili tanzania bara.

Audio Duration:
3'1"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud