Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa milimani kusaidiwa kukabili njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uhamiaji

Watu wa milimani kusaidiwa kukabili njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uhamiaji

Pakua

Serikali na asasi za kiraia zimeamua kushika usukani katika kuwasidia watu waishio milimani kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabia nchi, njaa na uhamiaji  kwa mujibu wa ripoti ya shirika la chakula na kilimo FAO iliyotolewa leo.

Ripoti hiyi inasema nchi takriban 60 na mashirika ya kiraia zaidi ya 200 wametoa ahadi leo katika siku ya kimataifa ya milima, kuimarisha uwezo wa watu wa milimani na mnepo wa mazingira yao wakati huu ambapo kuna ongezeko kubwa la athari za mabadiliko ya tabia nchi, njaa na matatizo ya uhamiaji ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya milima yanajumuishwa katika ajenda ya mwaka 2030 ya amendeleo endelevu au SDG’s.

Wanachama wa muungano wa ushirika wa milima ulioanzishwa mwaka 2002 na Italia, Uswis, FAo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP , na ukiwa na wajumbe zaidi ya 300 kutoka serikali mbalimbali, asas iza kiraia na sekta binafsi wameahidi kutekeleza hayo ifikapo 2030.

Ripoti hiyo ya FAO inasema serikali sasa zitatthimini upya será zake za maendeleo na kuzifanyia marekesho ili kujumuisha miakati inayohitajika, pia mashirika ya kimataifa, asas iza kiraia na sekta binafsi watatthjimini na kurekebisha será zao ikiwa ni pamoja na kushirikiana kuelimisha umuhimu wa kuwa na maendeleo endelevu ya milima.

Jumla ya watu bilioni moja wanaishi milimani takribani asilimia 13 ya watu wote, na mtu mmoja kati ya watatu  wanaoishi milimani kwenye nchi zinazoendelea anakabiliwa na matatizo ya uhakika wa chakula kutokana na majanga na mabadiliko ya tabia nchi.

Photo Credit
Wakulima wa Nepal wanabeba lishe ya mifugo. Picha: FAO