Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chukua hatua, simamia haki za binadamu:Zeid

Chukua hatua, simamia haki za binadamu:Zeid

Pakua

Leo ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa tarehe 10 ya mwezi Desemba. Mwaka huu ikiwa ni wa 69 tangu kupitishwa kwa azimio namba 2017  la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa hapo Desemba mwaka 1948, Kamisha mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Raa’d al Hussein ametoa ahadi ya kuhakikisha haki hizo zinapiganiwa na kuheshimiwa

“Zeid: Nitalinda haki zako bila kujali wewe ni nani, nitaheshimu haki zako hata kama sikubaliani na wewe. Wakati ambapo haki za binadamu za mtu yeyote zinakiukwa , haki za kila mtu zinapokuwa mashakani , nitazisimamia. Nitapaza sauti yangu , nitachukua hatua, nitatumia haki zangu kupigania haki zako”

Zeid pia amechagiza kila kila nchi na kila mtu kuhakikisha mkataba wa haki za binadamu unatekelezwa kwa videndo na sio kwa maneno hasa katika wakati huu ambao dunia imeghubikwa na ukiukwaji mkubwa  wa haki kwa kila namna , kuanzia misingi ya rangi, ukabila, utaifa, kwa visingizio vya kupambana na ugaidi, misingi ya kisiasa, dini na hata kwa maslahi binafsi. Hivyo amesema ni wakati wa kila mtu kuchukua hatua na kusimamia haki za binadamu katika jamii zinalindwa na kuheshimiwa.

Leo hii Umoja wa Mataifa mjini umezindua kampeni ya mwaka mzima ya kuenzi misingi ya azimio hilo la haki za binadamu ambayo itakwenda hadi Desemba mwaka 2018 wakati ambapo azimio hilo litatimiza miaka 70.

Photo Credit
Eleanor Roosevelt wa Marekani akiwa ameshika nakala ya tamko la haki za binadamu lililoandikwa la lugha ya Kiingereza (Novembea 1949). Picha na UN