Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Apu na mitandao ya kijamii yatoa nuru kwa wakimbizi wa Syria Uturuki:IOM

Apu na mitandao ya kijamii yatoa nuru kwa wakimbizi wa Syria Uturuki:IOM

Pakua

Wakimbizi wa Syria walioko nchini Uturuki wamefungua njia ya upatikanaji wa huduma za mtandao ambazo hutoa fursa ya upatikanaji wa habari za mahitaji ya jamii zao ili kuwasaidia kuanza maisha mapya.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji huduma hizo za app na mitandao ya kijamii zimewasaidia kupata haraka msaada kutoka kwa makampuni na mashirika ya kimataifa, na sasa zinasaidia jumuiya za watu waliotawanywa na machafuko kupata nyumba na kazi, tafsiri za sheria za Kituruki, ushauri wa kupata vibali vya makazi, kufungua akaunti za benki, na huduma zingine nyingi.

Kati ya wakimbizi milioni 3.3 wa Syria walioko Uturuki , takribani laki 220,000 wanaishi makambini wakipatiwa msaada wa makazi na huduma zingine za msingi na waliosalia wanaishi katika miji mikubwa ambako ni vigumu kupata ajira halali zitakazowawezesha kuishi wao na familia zao, hivyo wengi hugeukia teknolojia hususani mitandao ya kijamii na apu ambazo zinawasaidia kwa kiasi kikubwa.

Na kwa kulitambua hilo IOM hivi imeanza mafunzo ya teknolojia na mawasiliano (ITC) kwa wakimbizi hao ikishirikiana na makampuni mengine miongoni mwao ni kampuni ya simu ya Turkcell, Cisco, na mashirika yasiyo ya kiserikali au NGO’s kama Re:Coded na Natakallam.

Photo Credit
Khaled Fattal, mhandisi wa IT mwenye umri wa miaka 28, anashiriki katika warsha ya IOM kuhusu mipango ya ITC kusaidia usawa na ajira kati ya idadi ya watu waliokimbia makazi huko Gaziantep, Uturuki. Picha: IOM