Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye nuru yaangukia wapemba waliohamia Kenya

Hatimaye nuru yaangukia wapemba waliohamia Kenya

Pakua

Ukosefu wa taifa ni tatizo linalokumba mamilioni ya watu duniani. Wengi wao wakikosa utaifa kwa misingi ya dini, kabila au eneo walikotoka. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema mamilioni ya watu hawana utaifa na asilimia 75 ya kundi hilo ni watu kutoka makundi madogo. Ubaguzi, kutengwa na mateso ni mambo wanayokumbana nayo kila siku. Zahma hizo zinasababisha wakose haki yao ya msingi na ndio maana lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka jamii jumuishi na zenye amani. Kipengele cha 9 cha lengo hilo ndio kinaweka bayana haki ya kila mtu kupatiwa utambulisho ifikapo mwaka 2030. Je hali ikoje nchini Kenya kwa wapemba walioingia nchini humo kutoka Tanzania. Joshua Mmali anafafanua katika makala hii.

Photo Credit
Shaame Hamisi, Mvuvi mwenye umri wa miaka 55 ni mwenyekiti wa Wapemba waliohamia Kenya. Picha: UNHCR/Video capture