Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dkt. Salim azungumzia hatma ya Mashariki ya Kati

Dkt. Salim azungumzia hatma ya Mashariki ya Kati

Pakua

Kufuatia mjadala unaoendelea kuhusu hatma ya mji wa Yerusalem huko Mashariki ya Kati na mustakhbali wa suluhu ya mataifa mawili ya Palestin na Israel kwenye ukanda huo, mwanadiplomasia nguli nchini Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim ametaja kile kinachopaswa kuzingatiwa ili amani iwepo.

Dkt. Salim ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, UNIC baada ya mazungumzo yake na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za msingi kwa watu wa Palestina, Dkt. Salim jijini Dar es salaam.

(Sauti ya Dkt. Salim Ahmed Salim)

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema suluhu pekee ya mzozo Mashariki ya Kati ya Palestina na Israeli ni uwepo wa mataifa mawili akisema hakuna mbadala wa hilo.

Photo Credit
Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za msingi za wapalestina ilipokutana na mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez jijini Dar es salaam. (Picha:UNIC Dar es salaam/Lauren Kiiza)