Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa kike wang’ara utafiti wa kujua kusoma- UNESCO

Watoto wa kike wang’ara utafiti wa kujua kusoma- UNESCO

Pakua

Zaidi ya asilimia 96 ya watoto wenye umri wa miaka ya kati ya 9 hadi 10 wanajua kusoma

Ripoti ya utafiti wa zaidi ya nchi 50 duniani uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO umeonyesha kuwa watoto wa kike wanaongoza zaidi kuliko wa kiume.

Nchi ya Urusi imeongoza katika utafiti huo ikifuatiwa na Singapore, Hong Kong, Ireland, Finland na Poland.

Utafiti huo uliofanywa na wataalamu wa UNESCO  kwa kushirikiana na wadau wengine wa elimu ni wa kwanza kufanyika na pia uliangalia kiwango cha kujua kusoma kupitia mitandao.

Matokeo yameonyesha kuwa wasomi wazuri wa vitabu wana uwezo mzuri wa ufahamu wa stadi za kidijitali ambapo asilimia 50 ya wanafunzi walibainika kuwa ni wajuzi wa kusoma mitandaoni.

Utafiti pia umegundua kuna idadi kubwa ya watoto wanaojua kusoma vizuri kwa sasa ikilinganisha na miaka 15 iliyopita huku nchi 29 zikipanda na 12 zikishuka.

Photo Credit
Watoto wa kike wang’ara utafiti wa kujua kusoma. Picha: UNESCO