Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aibu ya mshtakiwa ni aibu yake na si jamii - ICTY

Aibu ya mshtakiwa ni aibu yake na si jamii - ICTY

Pakua

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kimbari katika iliyokuwa Yugoslavia, ICTY, Serge Brammetz ametaja kile kinachopaswa kufanyika ili kuleta maridhiano kamili kutokana na uhalifu uliotokea kwenye eneo hilo.

Amesema hayo akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kufuatia madai ya baadhi ya watu ya kwamba mahakama hiyo bado haijafanikiwa kuleta maridhiano kutokana na machungu ambayo wananchi wamepitia.

Bwana Brammets amesema baadhi ya washtakiwa wa uhalifu wa kivita bado wanaendelea kuvinjari na kuonekana ni mashujaa huku waathirika wakiumia..

(Sauti ya Serge Brammetz)

“Ukweli ni kwamba hakuna utashi wa dhati ndani ya ukanda husika katika kukubali makossa yaliyopita na kusonga mbele. Kibaya zaidi utashi huo haupo miongoni mwa uongozi wa kisiasa. Na jambo la kusikitisha ni kwamba watu wengi wanawasikiliza wahalifu wa kivita ambao wanajificha katika pazia la uwajibikaji wa pamoja wa wao na jamii zao katika makosa yaliyofanywa na washtakiwa hao..”

Amesema kwa misingi hiyo baadhi ya washtakiwa wanafichwa na hawaripotiwi kwa vyombo husika kwa kuwa jamii inaamini kuwa aibu ya washtakiwa hao ni aibu yao pia hivyo amesema..

(Sauti ya Serge Brammetz)

“Tofauti na hivyo tumekuwa tunasisitiza kuwa uhalifu huo haukutekelezwa na mataifa au watu, bali na mtu mmoja mmoja na wengi wao ni maafisa waandamizi wa kisiasa na kijeshi. Kwa hiyo hebu niweke wazi kuwa hakuna jamii inayobeba wajibu wa kile ambacho watu wake walitekeleza. Ndio maana ijapokuwa haki pekee haiwezi kufanikisha maridhiano lakini ni kigezo muhimu.”

 

Photo Credit
Rais Kolinda Grabar-Kitarović, wa Croatia (kushoto) akisaliamiana na mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu uliotokea kwenye iliyokuwa Yugoslavia, Serge Brammertz kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa New York, Marekani. (