Mtembea bure si sawa na mkaa bure- Millard Ayo
Pakua
Vijana ni nguvu kazi inayotegemewa katika kuboresha mustakabali wa dunia. Hata hivyo suala la ajira limekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa kundi hilo katika maeneo mbalimbali duniani. Yaelezwa kuwa idadi kubwa ya vijana wanapomaliza shule huishia kufanya kazi zisizokuwa na tija katika maisha yao ilhali wanaweza kupata fursa an ujuzi kwa njia tofauti na kuboresha maisha yao kama anavyoeleza Millard ayo kijana kutoka Tanzania ambaye anasema mwanzo wake ulikuwa na shubiri lakini bidii ndio imemwezesha kuchomoza na kujipatia umaarufu. Katika makala hii Patrick Newman alizungumza na Millard Ayo wakati alipotembelea Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjiin New York, Marekani na anaeleza kile alichofanya.