Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu huru wa UM kuzuru Korea Kaskazini

Mtaalamu huru wa UM kuzuru Korea Kaskazini

Pakua

Mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Korea Kaskazini Tomás Ojea Quintana  atakuwa na ziara maalum ukanda wa Asia kukusanya taarifa kuhusu maendeleo katika masuala ya haki za binadamu.

Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema ataanzia Korea Kaskazini tarehe 11 hadi 14 mwezi huu na badaye kuelekea Korea Kaskazini na hatimaye Japan kuanzia tarehe 15 hadi 16.

Ziara hiyo inafuatia kuzuka kwa hofu katika ukanda wa kaskazini-mashariki wa bara la Asia baada ya Korea Kaskazini ijulikanayo pia kama Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK, kufanya majaribio makombora ya masafa mrefu.

Tangu kuanzishwa kwa nafasi ya mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa DPRK mwaka 2004, nchi hiyo haijatoa kibali cha ziara ili mhusika aweze kufanya ziara kwenye taifa hilo.

Hata hivyo hivi karibuni DPRK imeruhusu mtaalamu huyo kuwa na mazungumzo nchini  humo na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Bwana Quintana atawasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa mwezi machi mwakani.

Photo Credit
Mjumbe maaalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Korea kaskazini Tomás Ojea Quintana. Picha: UM/Jean-Marc Ferré