Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu katika kufanikisha SDG’s:UNOSSC

Ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu katika kufanikisha SDG’s:UNOSSC

Pakua

Wakati nchi nyingi zinazoendelea zikiunda suluhu na miradi itakayoweza kutumiwa pia na watu wengine na wakati huohuo kuwa na fursa zaidi za kufanya uwekezaji wa kibiashara na uhamishaji wa teknolojia miongoni mwao, ushirika wa Kusini-Kusini unazidi kuwa muhimu katika kufikia ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDG’s.

Hayo yamesemwa na Jorge Chediek, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ushirika wa Kusini-Kusini (UNOSSC). Leo tamasha la kimataifa la maendeleo la Kusini-kusini 2017 (GSSD) likianza mjini Antalya Uturuki , Bwana Chediek amesema litatoa jukwaa muhimu la kubadilishana mbinu bunifu za suluhu kwa ajili ya changamoto za maendeleo zinazojitokeza katika nchi za Kusini-Kusini.

 (CHEDIEK CUT)

“Ni tamasha la tisa na kila mwaka watu wanabadilishana uzoefu zaidi na mafanikio na kudhihirisha kwamba nchi za Kuisini-kusini zinapata suluhu za changamoto zao zenyewe na zina hamasa ya kuwajuza wengine, sababu ushirika wa Kusini-Kusini ni muhimu katika kusaka suluhu ya changamoto za maendeleo kwa nchi zinazoendelea na malengo ya SDG’s yanahitaji muungano wa kimataifa na ushiriki wa nchi zote.”

Na hivyo

(CHEDIEK CUT 2)

“Ushirika wa Kusini-Kusini usionekana kama mbadala bali msaada wa kutia motisha ushirika wa Kaskazini-Kusini, lakini utakaokuwa muhimu sana kwa sababu unaweza kuzalisha na kutoa ujuzi muafaka na mifano halisi kwa ajili ya nchi zingine zinazoendelea.”

Ameongeza kuwa la msingi hapa ni kwamba ushirika wa Kusini-Kusini unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kufikia SDG’s hasa kwa kuboresha uwezo wa uzalishaji, kufanikisha biashara na uwekezaji na kushirikiana teknolojia muafaka.

Watu zaidi ya 1100 kutoka nchi zaidi ya 120 wanaohudhuria na kushiriki katika matukio zaidi ya 35 kwenye tamasha hilo.

Photo Credit
Bwana Jorge Chediek, mwakilishi wa Katibu Mkuu na mkuu wa ofisi ya ushirika wa Kusini-Kusini UNOSSC. Picha na UM