Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM ‘waibana koo’ Myanmar

UM ‘waibana koo’ Myanmar

Pakua

Serikali ya Myanmar imepewa miezi sita kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ripoti maalumu ya hali ya wanawake na wasichana wa kabila la Rohingya kutoka jimbo la kaskazini la Rakhine.

Uamuzi huo umetolewa na kamati ya mkataba wa kimataifa wa kutokomeza ubaguzi wa aina zote dhidi ya wanawake, CEDAW huko Geneva, Uswisi, kama yenye jopo la wataalamu 23 wa Umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo imetakiwa kueleza kwa kina mambo kadhaa ikiwemo idadi ya wanawake na wasichana waliobakwa, waliokufa, nani aliyetoa amri ya kutekelezwa kwa matukio ya ukatili, na hatua zilizochukuliwa .

Waraka wa kutakiwa kuwasilisha ripoti hiyo umewasilishwa kwa serikali yaMyanmar jana jumatatu ambapo hadi kufikia tarehe 28 mwezi Mei mwakani Myamar inatakiwa iwe  imewasilisha ripoti hiyo.

Tangu kamati hiyo ianze kufanya vikao vyake mwezi Oktoba mwaka 1982, hii ni mara ya nne kuomba ripoti mahsusi kutoka kwa nchi mwanachama.

Photo Credit
Khadija, msichana MRohingya mwenye umri wa miaka 16 anasimulia kilichomkuta kabla ya kukimbia. Picha: UM/Video capture