Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japo tauni imedhibitiwa Madagascar tuendelee kuchukua tahadhari :WHO

Japo tauni imedhibitiwa Madagascar tuendelee kuchukua tahadhari :WHO

Pakua

Mlipuko wa ugonjwa wa tauani umedhibitiwa nchini Madagasacar lakini ni lazima hatua ziendelee kuchukuliwa ili kuhakikisha mlupuko huo hautokei tena na kusambaa limeonya leo shirika la afya ulimwenguni WHO.

Akisisitiza kuhusu hilo mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema zahma imekwisha lakini ni lazima kuwa tayari kubaini na kudhibiti maambukizi mapya mpaka msimu wa tauani utakapoisha Aprili 2018.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na wizara ya afya ya Madagascar idadi ya maambukizi mapaya inaendelea kupungua katika wiki za karibuni hali inayoashiria kwamba hatua zilzochukuliwa kukabiliana na mlipuko huo zimefanya kazi ingawa maambukizi zaidi yanatarajiwa mpaka utakapomalizika msimu.

Dr Tedros ameipongeza serikali ya Madagascar kwa jinsi ilivyoshirikiana na wadau kudhibiti mlipuko huo. Tangu Agosti Mosi na Novemba 22 wizara ya afya ya nchi hiyo iliorodhesha jumla ya visa 2348, vikiwemo vifo 202, na karibu watu wote walipatiwa matibabu bure.

Ameongeza kuwa ni zahama kwamba ugonjwa wa enzi hizo ambao unaweza kutibika kirahisi unaweza kutishia usalama wa nchi nzima na kuua watu zaidi ya 200.

Tangu kulipuka kwa ugonjwa huo WHO na mtandao wa kimataifa wa tahadhari na kupambana na magonjwa ya mlipuko (GOARN) wamepeleka Madagascar zaidi ya wafanyakazi 135 kusaidia

Photo Credit
Tauni na jinsi inavyoenezwa. Picha: WHO