WFP yapokea dola milioni moja kutoka China kusaidia wakimbizi Iran
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 1 kutoka China kwa ajili ya chakula na pia vifaa vya elimu kwa wasichana wakimbizi wa Afghanistan na Iraq wanaoishi nchini Iran.
Negar Gerami ambaye ni mwakilishi wa WFP Iran amesema mchango huo ambao umefika muda muafaka utasaidia kuongeza chakula kama vile mchele, unga wa ngano kwa ajili ya wakimbizi elfu 30 ambao hutegemea sana msaada kutoka WFP katika kujikimu mahitaji mbalimbali.
Kwa upande wake China imesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa mfuko wa usaidizi wa ushirikiano wa Kusini-Kusini uliotangazwa na Rais wa China Xi Jinping katika mkutano wa uendelezaji wa Umoja wa Mataifa wa Septemba 2015, ikiwa ni jitihada za usalama wa chakula kwa wakimbizi walioathirika sana nchini Afghanistan katika Iran.