Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki kwa pande zote ni suluhu ya amani ya kudumu Iraq

Haki kwa pande zote ni suluhu ya amani ya kudumu Iraq

Pakua

Serikali ya Iraq lazima ihakikishe ushindi wa kijeshi dhidi ya wanamgambo wa ISIL unaenda mbali zaidi na kuhakikisha uwajibikaji na kuachana na ukwepaji sheria.

Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji kinyume cha sheria Agnes Callamard, baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi nchini Iraq.

Amesema wakati huu ambapo vitisho vya kijeshi kutoka ISIL vimepungua, nchi hiyo sasa inaingia kipindi cha mpito ambacho ingawa ni kigumu na tete  bado ni fursa ya kuachana na yaliyopita.

Hata hivyo Bi. Callamard amesema kuna hatari ya visasi vya zamani kuibuka tena kama hatua hazikuchukuliwa kuepusha hali hiyo.

Kwa mantiki hiyo ametaka serikali ihakikishe mambo yote yaliyokuwa yanababisha mauaji kinyume cha sheria ikiwemo yale ambayo hayakuhusiana na mzozo yanachunguzwa na wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Photo Credit
Wanawake, wanaume na watoto wapoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya ISIL. Picha: UM