Wanawake wajasiriamali wanahitaji fursa, sio zawadi

Wanawake wajasiriamali wanahitaji fursa, sio zawadi

Pakua

Katika jitihada za kukuza biashara zao, wanawake wajasiriamali wanatafuta fursa na sio kusubiri kupewa zawadi, amesema afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO.

Adot Killmeyer-Oleche, mkuu wa taasisi ya UNIDO na uwezeshaji wa maendeleo ameyasema hayo katika majadiliano kuhusu wanawake na viwanda yanayofanyika mjini Manama Bahrain kama sehemu ya jukwaa la kimataifa la uwekezaji na ujasiruiliamali kwa ajili ya maendeleo.

Wakati wa mjadala huo wanawake wamiliki wa biashara kutoka sehemu mbalimbali duniani wamebadilishana mawazo kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo kuanzia fursa ya kupata mitaji, teknolojia, unyanyapaa na vizingiti vya kijamii.

Bi Killmeyer-Oleche amesisitiza

(ADOT CUT)

“Wanawake sio watu wasio na uwezo, wote wanataka kutimiza ndoto zao, wanafanya bidii sana kufikia malengo yao ya biashara , na nafikiri hii ni fursa kwa watunga sera wote, kwa wawekezaji kwa watu wanaomiliki teknolojia, kutambua kwamba wanatafuta fursa na sio zawadi.”

Photo Credit
Mwanamke mjasiriamali nchini Senegal.(Picha:UNIDO/Video Capture)