Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji na usafi ni changamoto kwa wakimbizi wa Rohingya: IOM

Maji na usafi ni changamoto kwa wakimbizi wa Rohingya: IOM

Pakua

Upatikanaji wa maji safi na mazingira ya usafi ndio changamoto kubwa inayowakabili wakimbizi wa Rohingya waliongia Bangladesh kutokea Myanmar limesema leo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Tangu tarehe 25 Agosti zaidi ya wakimbizi wa Rohingya 600,000 wamevuka mpaka na kuingia Bangladesh. IOM inasema ingawa kasi ya idadi ya wakimbizi wapya wanaoingia inapungua, lakini bado watu wanaendelea kuwasili katika makazi ya Cox’s Bazar  kila siku na kufanya jumla ya Warohingya walio katika wilaya hiyo kuzidi 820,000.

Shirika hilo linasema makazi ya Cox’s Bazar yamefurika na kusababisha shinikizo kubwa la rasilimali muhimu za maji safi na usafi. Na wakimbizi wengi wanaowasili wanakuwa hoi kwa uchovu na kuumwa baada ya kutembea kwa siku kadhaa bila chakula na maji.

Photo Credit
IOM imechimba visima 14 vya pampu za mkono katika makazi ya Cox Bazar tangu Agosti 25, 2017. Wanaochota maji ni wakimbizi waRohingya. Picha: IOM