Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yafunga rasmi vituo 11 Darfur, Sudan

UNAMID yafunga rasmi vituo 11 Darfur, Sudan

Pakua

Mpango wa pamoja Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur nchini Sudan UNAMID, umefunga rasmi vituo kumi na moja hii leo huko Darfur na kuvikabidhi rasmi kwa serikali ya Sudan katika kutimiza makubaliano ya azimio la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 2363 la mwaka 2017.

Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na mwakilishi maalumu wa pamoja wa UNAMID Jeremiah Mamabolo, inachukua awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ikiwa ni kupunguza uwepo wa askari hadi 11,395 na polisi hadi 2,888 katika eneo la Magharibi mwa Sudan katika kipindi cha mwaka mmoja.

Vituo vilivyofungwa ni Tulus, Forbaranga, Tawila, Muhageria, Habila, Abu Shouk, Malha, Mallit, Umkadada, Tina na Zam Zam. Hatua hiyo ikitajwa kama ishara ya kurejea kwa hali ya utulivu katika jimbo la Darfur.

UNAMID baada ya kutia saini stakabadhi za kurejesha rasmi vituo hivyo kupitia Mamabolo na kuvikabidhi kwa serikali ya Sudan, imependekeza kwamba vituo hivyo vitumike katika kuendeleza jamii kwa kuzingatia matakwa ya jamii.

Photo Credit
Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anashusha bendera ya UM kama ishara ya kunguwa kwa kituo. Pembeni ni maafisa wa UM na serikali ya Sudana waliohudhuria sherehe hizo. Picha: UNAMID/Video capture