Skip to main content

Iran izingatie ahadi zake ili JCPOA iwe endelevu- Amano

Iran izingatie ahadi zake ili JCPOA iwe endelevu- Amano

Pakua

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa Yukiya Amano hii leo amezuri Iran ambako amekuwa na mazungumzo na viongozi waandamizi wa nchi hiyo akiwemo Rais Hassan Rouhani.

Ziara hiyo inafuatia mpango wa shirika hilo ambalo tangu mwezi Januari mwaka 2016 limekuwa likithibitisha na kufuatilia ahadi za Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia sanjari na makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, JCPOA.

Ahadi hizo ni kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa  Mataifa ambapo Iran inatakiwa kuzingatia vigezo vya kuhakikisha mpango wake wa nyuklia unakidhi vigezo vya kimataifa vya usalama.

Wakati wa mazungumzo na viongozi hao waandamizi, Dkt. Amano amesisitiza umuhimu wa Iran kuhakikisha inatekeleza ahadi hizo na kwamba mkataba wa kimataifa wa mpango wa nyuklia kuhusu Iran, JCPOA unawakilisha manufaa ya mpango huo wa ufuatiliaji.

Kwa mantiki hiyo amesihi Iran itekeleze wajibu wake ili JCPOA iwe endelevu.

Photo Credit
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Dkt. Yukiya Amano (Picha:D. Calma/IAEA)