Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikishwaji wa mwanamke kuchagiza amani na usalama ni lazima-Phumzile

Ushirikishwaji wa mwanamke kuchagiza amani na usalama ni lazima-Phumzile

Pakua

Ushirikishwaji wa wanawake katika kuchagiza amani na usalama wa kimataifa ni suala la lazima na sio hiyari.

Msisitizo huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women Phumzile Mlambo-Ngucuka kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wakati wa mjadala wa wazi wa kila mwaka kuhusu wanawake, amani na usalama.

image
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka
Katika mjadala huo uliojikita katika utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya baraza la usalama yanayohusu mada hiyo na pia kubainisha mapengo na changamoto zilizopo katika utekelezaji, bi Ngcuka amesema kuna hatua zilizopigwa katika kuwawezesha wanawake kisiasa, kiuchumi, kuwashirikiana katika mustakhbali wa nchi na kudhibiti ukatili dhidi ya wanawake katika maandishi

(Sauti ya Phumzile )

“uovu dhidi ya wanawake na wasichana katika vita vya silaha haujawahi kuorodheshwa ipasavyo kama sasa, mahakama za uhalifu za kitaifa na kimataifa, uorodheshaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu na juhudi za kuweka nyaraka za visa zinazoongozwa na asasi za kiraia , wataalamu na waandishi wa habari zinatoa kipaumbele kwa  ukatili wa kingono na kijinsia dhidi ya wanawake hivi sasa kuliko hapo nyuma.”

Hata hivyo ameongeza kuwa pamoja na hatua zote hizo zilizopigwa na visa vyote vilivyoorodheshwa vya ukatili tunapungukiwa

(Sauti ya Phumzile)

“Ambacho hatua ni uwajibikaji kwa watekelezajiwa uhalifu huo, haki na utu na msaada kwa manusura, ukwepaji huu wa sheria ni lazima ukome.”

Amesisitiza kuwa mshikamano wa kimataifa unahitajika ili kuhakikisha kila nchi inatekeleza maazimio yaliyowekwa na kuzingatia sheria na juhudi zinakuwa kwa vitendo na sio katika nyaraka.

Photo Credit
Walinda amani wanawake wakizunugmza na wanawake wanajamii eneo la Ntoto Kivu Kaskazini.(Picha:MONUSCO)