WFP yatoa wito kufikia maeneo yaliyozingirwa kunakoshuhudiwa njaa Syria

WFP yatoa wito kufikia maeneo yaliyozingirwa kunakoshuhudiwa njaa Syria

Pakua

Uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo ya Mashariki mwa Ghouta katika vijiji vya Damascus Syria, umepungua mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana, na hivyo kuwaacha makumi ya maelfu ya watu bila msaada.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la mpango wa chakula duniani WFP mara ya mwisho kufikia eneo hilo ni Septemba lakini kufikia sasa ni watu 70,000 tu ndio wamepokea msaada wa chakula miongoni mwa watu takriban 400,000.

WFP na wadau wengine wako tayari kuwasilisha misaada ya dharura na kutathmini mahitaji iwapo watahakikishiwa usalama wao.

Kwa mantiki hiyo, WFP imetoa ombi la kuweza kufikia maeneo walioko mamilioni ya watu walio na mahitaji kote nchini, bila kujali waliko.

Takriban watu 420,000 wanaishi katika maeneo yaliyozingirwa Syria na wengi wao wako Mashariki mwa Ghouta ambako chakula ni kidogo na ni vigumu kufikia.

Photo Credit
Raia wakipokea msaada wakibinadamu nchini Syria. Picha: UNHCR