Hispania kushirikiana na UM katika kampeni ya usafi wa bahari
Serikali ya Hispania imetangaza rasmi leo kuunga mkono Umoja wa Mataifa katika kampeni ya usafi wa bahari katika hafla ya mashindano ya bahari yajulinkanao kama Volvo ocean Race, yaliofanyika Alicante.
Bw.Raquel Orts Nebot, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya maendeleo ya pwani na Bahari nchini Hispania amethibitisha jitahada za taifa hilo kubwa na muhimu duniani kujiunga na nchi zingine 32 katika kampeni ya umoja wa mataifa ya usafi wa bahari. Bw Raquel amesma serikali yake itakuwa mtari wa mbele katika kuzihimiza nchi zingine na asasi za kiraia katika kupunguza matumizi ya plastiki baharini.
Naye Erik Solheim mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingiria UNEP amesema ushiriki wa Hispania katika kampeni hii unatuma ujumbe muhimu ukanda wa mediterranean na duniani kote. Ameongeza kuwa kama binadamu tuna wajibu wa kulinda bahari maana ni muhimu kwa maisha yetu .
Ripoti ya UNEP inasema uzalishaji wa plastiki umefikia zaidi ya tani bilioni 8.3 duniani kote, na mwaka 2015 tani bilioni 6.3 tayari zimetupwa, hivyo tani milioni 8 zinatupwa katika bahari zetu kila mwaka.
Watalaamu wanasema uchafuzi mwingi unajumuisha plastiki kama vikombe, mifuko, majani, chupa na vipodozi... Na ifikapo mwaka 2050 imeelezwa kuwa kutakuwa na plastiki zaidi katika bahari kuliko samaki.