Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa kiuchumi duniani unatumainisha

Ukuaji wa kiuchumi duniani unatumainisha

Pakua

Shirika la fedha duniani, IMF limetangaza leo ukuaji thabiti wa uchumi duniani lakini limesema doa katika ukuaji na wasiwasi kuhusu madeni inamaanisha kwamba watunga sera hawapaswi kubweteka.

Akizungumza kuhusu utabiri huo Mkurugenzi wa kitengo cha utafiti Maury Obstfeld amesema IMF imeridhishwa na utabiri ulioimarika kwa asilimia moja katika ripoti yake ya hali ya kiuchumi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ukuaji thabiti katika maeneo ya Ulaya, Japan, mataifa yanayoibuka ya Asia, na Russia yanachangia katika ukuaji huo tofauti na Marekani na Uingereza.

Hatahivyo bwana Obstfeld ametoa onyo kwamba licha ya hali hii kuna hatari za kisiasa na pia mabadiliko ya bei ya bidhaa, pia kuna hatari ya mitaji isiyotabirika wakati benki kuu zikirejelea hali ya kawaida na kuimarika kwa dola ya Marekani.

Aidha ameongeza kwamba hatari kubwa zaidi ni watunga sera kutumia fursa hii kufanya mabadiliko makubwa

(Sauti ya Obstfeld)

“Tuna furaha sana kwa kuongezeka kwa mwelekeo wa ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu na kwa asilimia moja katika kila mwaka. Tunatarajia ukuaji wa mwaka huu kufikia asilimia 3.6  na 3.7 mwaka ujao.”

Photo Credit
Mkurugenzi wa kitengo cha utafiti, IMF Maury Obstfeld. Picha: UM/Video capture