Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia kuwapa makazi waathirika wa kimbunga Dominica

IOM yasaidia kuwapa makazi waathirika wa kimbunga Dominica

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linasaidia waathirika wa kimbunga Maria kilichopiga visiwa vya Jamhuri ya Dominica kupata makazi. IOM imesema wiki tatu tangu kimbunga Maria, kukumba visiwa vya Carribea wakaazi wanamahitaji ya muhimu ya maji, umeme, na mahitaji mengine. Hatahivyo mahitaji ya dharura ni makazi.

Kulingana na ripoti za IOM asilimia 23 ya nyumba 26,000 zimesombwa na kuelekezwa baharini au kusambaratika kabisa. Aidha asilimia 39 zimeharibiwa na asilimia 28 zimeathirika kwa kiasi fulani.

IOM imeongeza kuwa idadi hiyo ni ishara ya hali ya uchungu ya maisha katika makazi mengi ambako zaidi ya watu elfu mbili wa Dominica wanaishi huku wengine wakipata msaada kwa kuishi na jamaa na marafiki.

Photo Credit
(IOM) 2017