Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sayansi ya nyuklia ina dhima muhimu katika maendeleo- Amano

Sayansi ya nyuklia ina dhima muhimu katika maendeleo- Amano

Pakua

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la atomiki, IAEA Yukiya Amano amesisitiza dhima ya shirika lake katika kuimarisha usalama wa nyuklia duniani kwa maendeleo.

Amano amesema hayo mjini Roma, Italia hii leo wakati wa mkutano wa 20 wa Edoardo Almadi ukiangazia ushirikiano wa kimataifa katika kuimarisha usalama wa nyuklia na kudhibiti kuenea kwa silaha hizo.

Mathalani ametaja ushirikiano wa muda mrefu kati ya IAEA na muungano wa Ulaya, EU katika usalama wa nyuklia akisema viwango vya udhibiti vya pamoja kati ya pande mbili hizo vimeimarisha usalama.

Dkt. Amano amesema ingawa usalama wa nyuklia ni wajibu wa kitaifa, bado IAEA inaweka vigezo ambavyo ndio msingi wa ushirikiano kati ya mataifa na shirika hilo, ushirikiano ambao pia unasongesha maendeleo.

Ametolea mfano usaidizi wa IAEA kwa nchi zinazoendelea kwenye sayansi ya nyuklia na teknolojia hususan uzalishajiwa chakula, umeme na tiba ya magonjwa akisema ushirikiano huo utaendelea kuimarishwa siku za usoni.

Photo Credit
Nchini Costa Rica, IAEA inasaidia nchi hiyo kutumia teknolojia ya nyuklia katika kutokomeza mbun'go ambao wanasababiisha magonjwa kwa wanyama. (Picha: L. Gil/IAEA)