Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa wasomali unazidi kudorora- Ripoti

Ustawi wa wasomali unazidi kudorora- Ripoti

Pakua

Benki ya Dunia hii leo imezindua ripoti ya kina kuhusu hali ya ustawi ya wananchi wa Somalia ikionyesha kuwa hali ya umaskini inakithiri kadri muda unavyosonga.

Ripoti hiyo inasema kila sekunde moja ya msomali ni maisha ya dhiki, kaya zikiendelea kukabiliwa na umaskini na uwezo wa kupata ajira ukipungua.

Kiwango cha umaskini kinachoainishwa na uwezo wa matumizi ni chini ya kiwango cha kimataifa cha dola 1.90 kwa siku.

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia, Bella Bird amesema suluhu pekee ni kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya ajira ili kuwa na uchumi endelevu.

Halikadhalika ripoti hiyo pia imeangazia umuhimu wa fedha zinazotumwa na ndugu na jamaa kutoka nje ya nchi ikisema zinasaidia kuondoa ufukara miongoni mwa familia.

Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo Utz Pape amesema ni kwa kuzingatia hali hiyo, ripoti hii mpya itasaidia watunga sera, watendaji wa serikali kuchukua hatua stahiki kupunguza umaskini.

Photo Credit
Wakimbizi wa ndani nchini Sommalia kufuatia ukame uliokithiri. Picha: UM/Stuart Price