Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto waliotawanywa na volkano Ambae wanahitaji msaada haraka:UNICEF

Watoto waliotawanywa na volkano Ambae wanahitaji msaada haraka:UNICEF

Pakua

Watu takribani 12,000 wako katika hatari kubwa ya volkano nchini Vanuatu wakiwemo maelfu ya watoto waliohamishwa kutoka  kisiwani Ambae na sasa wanahitaji msaada wa haraka kwenye vituo vya muda vilivyowekwa kwenye visiwa vya jirani.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambapo mwakilishi wake kwenye eneo la Pacifiki Sheldon Yett,  amesema kikubwa kinachotia hofu ni kwa maelfu ya watoto waliolazimika kukimbia makwao kuwa katika makazi salama.

Ameongeza kuwa chini ya uongozi wa serilikali ya Vanuatu UNICEF inajitahidi kuhakikisha watoto hao wanapata huduma za msingi ikiwemo maji safi na huduma za usafi mashuleni.

UNICEF inasema zaidi ya wanafunzi 3000 wakiwemo 2000 wa shule za msingi na 1000 wa sekondari hivi sasa hawako shuleni na wanahitaji kusajiliwa katika shule za jirani kwenye maeneo ya Maewo, Pentecost na kisiwa cha Santo

Photo Credit
Tamanu atazama vyombo vya upishi akitafakari maisha yake ya baadaye baada ya kuhamishwa. Picha (maktaba): © UNICEF Vanuatu/2015/Metois