Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yakarabati vituo vya kulinda raia eneo la WAU

UNMISS yakarabati vituo vya kulinda raia eneo la WAU

Pakua

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS na wadau wengine wanapanga upya maeneo ya ulinzi wa raia nchini humo kwa ajili ya kuimarisha usalama na hali ya maisha kwa watu wapatao 39,000.

Kwa sasa  eneo la ulinzi wa raia la Wau limerundikana watu kufuatia mapigano mapya mwezi Aprili mwaka huu.

Ashley Mclaughlin kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM amesema kumekuwa kumekuwa na idadi kubwa ya watu wanaomiminika kila uchao na 13,000 waliwasili WAU ambako kwa sasa hali ni mbaya wakati huu ambao kunashuhudiwa msimu wa mvua  huku kukiwa na hatari ya kusambaa kwa magonjwa ikiwemo malaria. Aidha

(Sauti ya Ashley)

“Wasi wasi mkubwa kwa sasa ni kupanga upya kituo hiki na makazi kwa njia ambayo watu wataweza kufikia huduma za kibinadamu, na kwamba ni salama, tunaweza kukarabati miundombinu ya maji taka na mambo kama hayo. Pia iwapo moto au kitu kama hicho kinazuka polisi wa Umoja wa Mataifa, walinda amni na watoa huduma wanaweza kukabiliana na matukio hayo.”

Polisi wa Umoja wa Mataifa, UNPOL na walinda amani wanapiga doria katika vituo hivyo ili kuhakikisha usalama. Stepehen Kirn, ni mratibu wa ulinzi wa vituo vya raia

(Sauti ya Kirn)

“Tunaimarisha doria kwa miguu na gari ndani ya kituo, pia tunafungua maeneo zaidi kwa ajili ya kuwafikia wakimbizi wandani kuweza kuingia na kutoka na kwa ajili ya operesheni za kutafuta vitu vinavyoingizwa ndani ya kituo, pia tunapiga doria kuhakikisha hakuna vitendo vya uhalifu ndani ya kituo.”

 

Photo Credit
Ukarabati unaendelea WAU. Picha: UM/Video capture