Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Tunisia kwa kubadilisha sheria ya ndoa kwa wanawake -Wataalam UM

Heko Tunisia kwa kubadilisha sheria ya ndoa kwa wanawake -Wataalam UM

Pakua

Wataalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamekaribisha hatua ya Tunisia ya kufuta tarehe 13 mwezi huu sheria inayozuia mwanamke muislamu kuolewa na mwanamume wa dini tofauti.

Wakikaribisha hatua hiyo, wataalam hao pia wamehimiza Tunisia kufanya mabadiliko mengi zaidi kukabiliana na ubaguzi wakisema hiyo ni hatua muhimu katika kuhakikisha usawa kati ya wanawake na wanaume kwani sheria hiyo ilikuwa inawadhibiti wanawake tu na haikuwazuia wanaume kuoa wanawake wasio waislamu.

Wataalamu hao wamesema hatua hiyo inatokana na harakati za miaka mingi za wanawake lakini wakatolea wito serikali kuendeleza juhudi za usawa huo kwa kukabiliana na vitendo vingine vinavyobinya haki za wanawake ikiwemo uhusiano wa familia, talaka, malezi ya watoto na sheria za urithi.

Photo Credit
Wanawake nchini Tunisia. (Picha:UN Women/Video capture)