Watu zaidi ya laki 8 wapata chanjo ya kipindupindu Nigeria:WHO

Watu zaidi ya laki 8 wapata chanjo ya kipindupindu Nigeria:WHO

Pakua

Kampeni ya chanjo ya kipindupindu imekamilika miwshoni mwa wiki katika eneo la Maiduguri na viunga vyake huko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwa kuwapa matone ya chanjo watu 844,000.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO kampeni hiyo imeendeshwa katika kambi za wakimbizi wa ndani Maiduguri pamoja na Jere, Mongunona na Dikwa na shirika hilo limehakikisha kila mtu amefikiwa katika maeneo hayo.

Hadi kufikia leo WHO inasema visa 3934 vya kipindupindu vikiwemo vifo 54 vimeripotiwa. Shirika hilo, wizara ya afya ya Nigeria na wadau wengine wanajitajidi kudhibiti kusambaa kwa mlipuko huo, lakini kwa mujibu wa msemaji wa WHO Geneva Tarik Jasarevic, kuna changamoto katika baadhi ya maeneo.

(SAUTI YA TARIK)

“Kutokuwepo usalama ni changamoto kubwa, hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya mwafanyakazi wa misaada. Kuweza kufika katika baadhi ya maeneo kunahitaji kusindikizwa na askari katika barabara mbovu au kutumia helkopta, na mawasiliano katika maeneo mengi ni madogo sana.”

Photo Credit
© UNFPA / Anne Wittenberg