Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu ni tishio kubwa kwa wajawazito Nigeria: UNFPA

Kipindupindu ni tishio kubwa kwa wajawazito Nigeria: UNFPA

Pakua

Machafuko yaliyosababishwa na kundi la Boko Haram yamevuruga mfumo wa afya na usafi nchini Nigeria na kutawanya watu milioni 1.7 Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kwenye majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe.

Kwamujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, wengi wa watu hao wanaishi makambini au kuhifadhiwa katika jamii. Na mwezi wa Agosti mwaka huu mlipuko wa kipindupindu ukazuka kwenye jimbo la Borno na kutishia zaidi mustakhbali wa jamii ambazo tayari zinakabiliwa na zahma ya kibinadamu.

UNFPA inasema ugonjwa huo ambao unsababisha hatari ya watu kupungukiwa maji mwilini umewaweka wanawake hususani wajawazitio katika hatari kubwa. Dr Homsuk Swomen mtaalamu wa afya ya uzazi wa UNFPA huko Maiduguri amesema utafiti unaonyesha kwamba maambukizi ya kipindupindu wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha kupoteza mtoto ghafla, kujifungua njiti, kujifungua mtoto mfu na kuongeza hatari ya kifo kwa wote mama na mtoto.

Na kutokana na machafuko yanayoendelea ameongeza kuwa kina mama wengi wajawazito wana utapia mlo na hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa kipindupindu na maradhi mengine.

Photo Credit
Yana Duka ni mmoja wa waathirika 35 wa cholera katika kituo cha afya cha muda mfupi kambini Muna nchini Nigeria. Alipoteza mimba yake baada ya kuwa mgonjwa. Picha: © UNFPA/Anne Wittenberg