Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusaidiane kudhibiti utoroshaji wa fedha kutoka nchi maskini- Guterres

Tusaidiane kudhibiti utoroshaji wa fedha kutoka nchi maskini- Guterres

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uwezo wa nchi kujipatia mapato yake yenyewe ni moja ya mambo ya msingi katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu.

Amesema hayo wakati wa kikao cha kundi la nchi 77 na China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani akisema nchi maskini zinahaha kujikwamua lakini bado zinakumbwa na vikwazo..

 (Sauti ya Guterres)

“Ambacho bado tunashuhudia kwenye maeneo mengi, bara la Afrika ni mfano mzuri kwenye hili ni kwamba fedha inayotoroshwa nje ya bara hilo kwa njia ya utakasishaji wa fedha, ukwepaji kodi na usafirishaji haramu wa fedha,  ni kiasi kikubwa kuliko fedha zinazopelekwa kwenye bara la Afrika kama misaada rasmi ya maendeleo.”

Hata hivyo amesema nchi moja pekee haiwezi kupata suluhu ya ukwepaji kodi na usafirishaji haramu wa fedha kwa kuwa ni lazima jamii ya kimataifa iweke mfumo wa maadili wa kudhibiti na kutokomeza tabia hiyo, kwa hiyo..

 (Sautiya Guterres)

“Na hii inapaswa kuwa kipaumbele cha kazi yetu katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu.”

Photo Credit
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kikao cha kundi la nchi 77 na China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New YorkPicha: UM/Rick Bajornas