Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani kutoka Tanzania auawa DRC

Mlinda amani kutoka Tanzania auawa DRC

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mlinda amani kutoka Tanzania aliyekuwa anahudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO ameuawa huko Mamundioma jimbo la Kivu Kaskazini.

Taarifa  ya Umoja wa Mataifa imesema mauti yalimfika mlinda amani huyo ambaye hadi sasa jina lake halijatajwa huku mwenzake mmoja akijeruhiwa, kufuatia mapigano kati ya kikosi cha MONUSCO na wapiganaji wa kikundi cha ADF.

Kufuatia tukio hilo la Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Tanzania, ndugu na jamaa za mlinda amani huyo huku akimtakia ahueni majeruhi.

Ametoa wito kwa serikali ya DRC kufanya uchunguzi wa haraka ili wahusika wafikishwe mbele ya sheria.

Halikadhalika ametoa wito kwa vikundi vilivyojihami DRC kusitisha ghasia na kuepusha vitendo vitakavyozidi kuhatarisha hali ya amani na usalama nchini humo.

Photo Credit
FIB vikosi maalum vya Tanzania ambao wanahudumu katika sehemu ya MONUSCO, huko Sake, North Kivu (Maktaba). Picha: © MONUSCO / Sylvain