IOM yasaka fedha kusaida warohingya nchini Bangladesh

IOM yasaka fedha kusaida warohingya nchini Bangladesh

Pakua

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, linasaka zaidi ya dola milioni 26 ili kukidhi mahitaji ya haraka ya wakimbizi wapatao 313,000 wa Rohingya kutoka Myanmar.

Wakimbizi hao wanaishi katika maeneo saba ya wilaya ya Cox Bazar mpakani mwa Bangladesh na Myanmar.

IOM imesema msaada huu wa dharura wa miezi mitatu unahitajika sana ambapo mchakato unaonyesha kuwa dola milioni 15 pesa hizo ni kwa ajili ya malazi na chakula, milioni 5 zitakwenda kwenye huduma ya maji safi na usafi wa mazingira, milioni 3 itatoa ulinzi kwa watu wanaoishi kambini na dola 100,000 iliyobaki itatumika kwa shughuli za uratibu.

Naye Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bangladesh Robert Watkins amesema kabla ya mgogoro wa sasa kuanza, mashirika yalikuwa yanafanya kazi nchini kwa uwezo wa juu lakini sasa yamezidiwa uwezo.

Amesema wahitaji ni wengi kuliko uwezo wao hivyo usaidizi unahitajika hivi sasa.

Photo Credit
Wakimbizi kutoka Myanmar wapanga foleni kupokea misaada ya kibinadamu nchini Bangladesh. Picha: IOM