Wanyoro wa Uganda wahaha kuhifadhi asili yao

Wanyoro wa Uganda wahaha kuhifadhi asili yao

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linahimiza umuhimu wa kulinda tamaduni kwa ajili ya kuendeleza jamii na kukuza maelewano.

Aidha manufaa ya ulinzi wa utamaduni ni zaidi ya hapo kama inavyojitokeza katika makala hii kuhusu juhudi za kubaini maeneo ya kihistoria kwa ajili ya kuimarisha utalii sambamba na harakati za kusaka fidia kwa ukatili uliofanywa dhidi ya Wanyoro katika vita ya kupinga ukoloni wa Uingereza. Nchini Uganda. Basi ungana na John Kibego katika makala hii.

Photo Credit
Michezo ya kitamaduni kwenye kumbukumbu ya wahanga wa ukatili wa wakoloni kwenye kaburi la pamoja la Nalweyo. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili_John Kibego