Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yasema dhoruba Irma ni mwiba kwa watoto

UNICEF yasema dhoruba Irma ni mwiba kwa watoto

Pakua

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limetoa tahadhari kuhusiana na  dhoruba  Irma ambayo inakumba ukanda wa Karibea.

Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Amerika Kusini Marita Perceval  amesema  dhoruba hiyo ikiambatana na upepo mkali inatarajiwa kupiga eneo kubwa  la ukanda huo ikihusisha nchi za visiwani kama vile Antigua na Barbuda, Dominica, St. Maarten, St kitts na Nives pamoja na Haiti na Cuba ambako anasema maisha ya watoto yako hatarini.

Imgawa bado ni mapema kutathmini athari ambayo dhoruba hiyo Irma itasababisha ,  Bwana Parceval  amesema tatizo kuu kwa waathirika ambao wengi wao ni watoto ni pamoja na maji ya kunywa na chakula.

(Sauti ya Parceval)

“Jamii ya ukanda huu wa dhoruba Irma hususan Haiti  inatakiwa kujiandaa kuhahikisha kuna chakula na maji ya kutosha  kwa angalau siku tano zijazo .Vilevile wanatakiwa kuzingatia ushauri wa serikali kwa kuelekea kwenye maeneo yenye mwinuko yaliotengwa na serikali kwa jili ya kujihami na kimbunga IRMA.

Photo Credit
Kimbunga Matthew ilipitia Jeremie, Haiti, Octoba 4, 2016, nchi huu inajitayarisha kukabiliana na Kimbunga Irma. Picha: UM/Logan Abassi