UNHCR na Tanzania wabainisha hatua za kukabili suala la wakimbizi

UNHCR na Tanzania wabainisha hatua za kukabili suala la wakimbizi

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na serikali ya Tanzania watafanyia tathmini sera ya taifa hilo kuhusu wakimbizi ili kuhakikisha inakidhi hali ya sasa ya ukimbizi.

Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa kikao kati ya pande mbili hizo, kikao cha hivi karibuni zaidi cha ngazi ya juu kilichofanyika jijini Dar es salaam kikiangazia misingi ya ulinzi wa wasaka hifadhi na wakimbizi pamoja na hatua za pamoja za kuchukuliwa na pande mbili hizo.

Katika taarifa ya pamoja, UNHCR na Tanzania wamesema tathmini hiyo itawezesha kuwa na sera inayoruhusu utambuzi wa haraka wa wakimbizi wanaohitaji ulinzi.

Halikadhalika walijadili suala la wakimbizi wa Burundi kurejea makwao kwa hiari ambapo Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR Volker Turk ambaye alishiriki amesema kama ambavyo mtu anakimbizi nchi yake kwa hiyari na vivyo hivyo akitaka kurejea, suala ambalo litajadiliwa kwenye kikao cha pande tatu baadaya mwezi huu.

Tanzania inahifadhi wakimbizi zaidi 350,000 ambapo wengi wao wanatoka Burundi.

Photo Credit
Wakimbizi kutoka Burundi walioko nchini Tanzania. Picha: © UNHCR/K. Holt